Mshambuliaji Emmanuel Adebayor
amrejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kukamilisha uhamisho wa
kushtukiza kujiunga na Crystal Palace.
Klabu hiyo ya Crystal Palace
imethibitisha kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham aliyeachwa na
klabu hiyo amejiunga nao kwa mkataba hadi mwisho wa msimu huu.
Emmanuel Adebayor alikuwa akijifua
kujiweka fiti kwa muda wote wakati akitafuta klabu ya kuchezea.
M/Kiti wa Crystal Palace, Steve Paris akipeana mkono na Adebayor
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni