Uchunguzi wa kosa la kukwepa kodi
kwa klabu kubwa 35 za nchini Italia za daraja la kwanza umeanza
kufanyika.
Polisi wa nchi hiyo wa kikosi cha
masuala ya fedha wameanza kuendesha msako na kushikilia mali
zinazodaiwa kufikia euro milioni 12.
Kesi hiyo inahusisha watu 58 wa soko
la kulipwa, mwendesha mashtaka wa Naples amesema kwenye taarifa yake.
Mawakili wa klabu ya AC Milan
amesema makamu wa rais wa klabu hiyo Adriano Galliani ni miongoni mwa
wanaochunguzwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni