.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 19 Januari 2016

FASTJET YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA, MHANDISI SULEIMAN SAID SULEIMAN

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.

                SALAMU ZA RAMBIRAMBI

          Dar es Salaam, 19 Januari, 2016

Uongozi na wafanyakazi wa Fastjet Tanzania umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi  Suleiman S. Suleiman.

Tunaungana na familia, marafiki, ndugu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kutuma salamu za rambirambi katika kipindi hiki cha kuomboleza.

Fastjet Tanzania imefanyakazi kwa ukaribu na Mhandisi Suleiman na tunatambua mchango wake katika kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.

Tutaukosa kwa kiwango kikubwa ushauri, uongozi na ushauri wake kutokana na kifo chake. Tunaomba roho yake ipumzike kwa amani peponi.

                                    Imetolewa na Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni