Mwanasiasa wa Bavaria aliyeonyesha
kukerwa ametuma basi lililojaa wahamiaji 31 katika safari ya saa saba
kwenda kwenye ofisi ya Angel Merkel Jijini Berlin baada kumuonya
kiongozi huyo wa Ujerumani kuwa nchi imeelemewa na wahamiaji.
Wahamiaji hao walipakiwa kwenye basi
aina ya Coach, huko Landshut mji wa kusini wa Bavaria na gavana Peter
Dreir na kuwasafirisha maili 340 hadi katika mji mkuu wa Ujrumani,
Berlin.
Dreier ambaye ni mkosoaji wa sera za
Kansela Merkel za kuwapokea wahamiaji kwa kusema nchi hiyo imezidiwa
na wahamiaji, amesema alishamtahadharisha Kansela huyo mwezi Oktoba
mwaka jana.
Wahamiaji wakiwa wamepandishwa kwenye basi kwa safari ya kupelekwa ofisini kwa Kansela Angel Merkel



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni