Abiria wa ndege amepongezwa kama
shujaa baada ya kupambana kwa dakika 40 kuokoa maisha ya mwanaume
mmoja aliyepata shambulio la moyo wakati ndege ya Ryanair ikiwa
angani.
Abiria huyo mwanamke aliyekuwa
kwenye ndege iliyotokea kisiwa cha Canary kwenda Liverpool katika
uwanja wa John Lennon, alijitolea kuokoa maisha ya mwanaume huyo
baada ya kusikia tangazo la kuoamba msaada wa daktari.
Mwanamke huyo alinyanyuka na kwenda
kwenye kiti cha mwanaume aliyepatwa shambulio la moyo na kumsaidia
kuokoa maisha yake hadi ndege ilipotua Cork, Ireland kwa dharura.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni