.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 28 Januari 2016

HILLARY CLINTON KUMTEUWA RAIS OBAMA KUWA JAJI WA MAHAKAMA KUU

Muwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic Bi. Hillary Clinton amesema kumteuwa rais Barack Obama kuwa jaji wa mahakama kuu ni wazo zuri kabisa.

Akiwa katika kampeni zake huko Iowa, mpiga kura alimuuliza Bi. Clinton kama atafikiria kumteuwa rais Obama kuwa jaji wa mahakama kuu iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Bi. Clinton alikiri kuwa rais ajaye atapatiwa fursa ya kuwachagua majaji watatu wa mahakama kuu, na kumchagua rais Obama ni wazo zuri, ambalo hakuna mtu aliyewahi kupendekeza kwake hapo kabla.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni