.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 29 Januari 2016

HOFU YA ZIKA YAZIDI KUZUA MJADALA WA MICHUANO YA OLIMPIKI NCHINI BRAZILI

Michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio nchini Brazili inakabiliwa na hofu ya ongezeko la virusi vya Zika vilivyosababisha watoto 4,000 kuzaliwa na vichwa vidogo nchini humo.

Watanzamaji wanawake na wanariadha waliokatika umri wa kupata ujauzito wametahadharishwa na wataalam wa masuala ya afya duniani kufikiria vyema mipango yao ya kwenda Brazili kutokana na hofu ya watoto watakaowazaa kukabiliwa na ugonjwa huo.

Urusi na Australia wameonyesha hofu kwa wanamichezo wanawake wanaojiandaa kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio mwezi Agosti, huku mashirika kadhaa ya ndege yakiwapa fursa wanawake wajawazito waliokata tiketi kuhudhuria michuano hiyo kuziuza kwa watu wengine.
 Mtu akinyunyuzia dawa ya kuulia mazalia ya mbu katika moja la eneo la viwanja vya michezo
                      Daktari akimpima ukubwa wa kichwa mtoto aliyezaliwa nchini Brazil

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni