.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 28 Januari 2016

KUTOKA BUNGENI BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka ajali hiyo.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais. Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni