Luis Suarez amepachika mabao matatu
yaani hat-trick wakati Barcelona ikipambana kujaribu kutetea taji la
La Liga kwa kuitundika Athletic Bilbao iliyokuwa na wachezaji 10 kwa
mabo 6-0.
Bilbao walijikuta wakimpoteza
golikipa wao Gorka Iraizoz aliyetolewa nje mapema kwa kumuangusha
Suarez na kisha Lionel Messi kufunga kwa mkwaju wa penati.
Neymar alipachika bao la pili kabla
ya kipindi cha kwanza kumalizika, huku Suarez na Ivan Rakitic
wakifanya matokeo kuwa 4-0 katika kipindi cha pili. Suarez alifunga
bao la tano na la sita baadae.
Lionel Messi akijipinda kupiga shuti
Luis Suarez akipiga shuti la mpira wa kuzungusha
Matokeo mengine ya La Liga Valencia
2 - 2 Rayo Vallecano, Real Madrid 5 - 1 Sporting de Gijón, Getafe 3 - 1 Espanyol na Las Palmas 0 - 3
Atl Madrid.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni