.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 29 Januari 2016

MABONDIA KUTWANGANA DAR LIVE MARCH 12

Mabondia Iddi Mnyeke kushoto na Mohamed Kashinde wakiangaliana kwa usongo wakati wa utambuklisho wa mpambano wao utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA mbalimbali watazitwanga march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala akizungumza mbele ya waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo

Rajabu Mhamila 'Super D' amewasainisha mabondia mbalimbali kuzipiga siku hiyo ambapo bondia Ibrahimu Maokola 'Simba wa Mbagala' atazipiga na Joseph Sinkala kutoka Mbeya mpambano wa ubingwa raundi kumi kg 74 utakaosimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa 'TPBC' kinachongozwa na Rais Chaurembo Palasa

Aliendelea kwa kusema siku hiyo bondia Iddi Mnyeke kg 61 atamenyana na Mohamed Kashinde wakati Pius Kazaula kutoka Morogoro atakumbana na Karage Suba katika uzito wa kg 66

Wakati Shabani Kaoneka atakumbana na Said Seleman mpambano wa raundi sita kg 72 na Ambokile Chusa atavaana na Seleman Galile katika mpambano wa raundi sita kg 74

Pia kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayo sindikiza mpambano uho

Siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni