.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 24 Januari 2016

MANCHESTER UNITED WAZOMEWA BAADA YA KUCHAPWA NA SOUTHAMPTON


Mchezaji aliyetokea benchi Charlie Austin amefunga bao ndani ya dakika saba akiichezea kwa mara ya kwanza Southampton na kupelekea wachezaji wa Manchester United watoke dimbani wakizomewa na mashabiki wao baada ya kulala kwa bao moja kwa bila.

Austin aliruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliozaa goli akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa katika dakika ya 87, na kuifanya Southampton kuibuka na ushindi huo kwenye dimba la Old Trafford, katika mchezo huo uliokuwa na nafasi chacheza kufunga.

         Charlie Austin akiruka na kufunga mpira wa kichwa uliomshinda David De Gea 
Shambulizi la dakika za majeruhi la Adam Lallana limeifanya Liverpool kuibuka na ushindi katika mchezo uliokuwa hautabiriki na wakuvutia dhidi ya Norwich ulioshuhudia magoli tisa yakitinga wavuni.

Katika mchezo huo magoli ya Norwich yalifungwa na Mbokani Bezua 29′, Naismith 41′ Hoolahan 54′, (pen) Bassong 90′, huku ya Liverpool yakifungwa na Firmino 18′, 63′ Henderson 55′, Milner 75′ na Lallana 90′.

Dieumerci Mbokani akifurahia bao lake la kusawazisha alilolifunga kwa kisigino cha ufundi. Mchezo huo uliishia Liverpool 5-4 Norwich.

Matokeo Mengine ya Ligi Kuu ya Uingereza ni Crystal Palace 1 – 3 Tottenham, Leicester 3 - 0 Stoke, Sunderland 1 - 1 Bournemouth, Watford 2 - 1 Newcastle, West Brom 0 - 0 Aston Villa na West Ham 2 - 2 Man City.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni