Matokeo yaliyokuwa yanangojewa kwa
muda mrefu kuhusiana na kifo cha aliyekuwa jasusi wa Urusi, Bw.
Alexander Litvinenko yanatarajiwa kutolewa na Jaji.
Bw. Litvinenko alikufa akiwa na umri
wa miaka 43 Jijini London mwaka 2006, siku kadhaa kupita tangu
awekewe sumu ya mionzi ya polonium-210, ambayo inaaminika aliinywa
kwenye kikombe cha chai.
Watu wawili raia wa Urusi
waliotuhumiwa kuhusika na kifo hicho Andrei Lugovoi pamoja na Dmitry
Kovtun, wamekanusha kutenda kosa hilo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni