.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Januari 2016

POLISI AFRIKA KUSINI YACHUNGUZA VIFO VYA WATOTO KWENYE JOKOFU

Polisi nchini Afrika Kusini wameanzisha uchunguzi wa vifo vya watoto watano ambao wanadhaniwa walikufa kwa kukosa hewa baada ya kukutwa kwenye jokofu.

Watoto hao watano ndugu wenye umri wa kati ya miaka mitatu na saba, waligunduliwa na Bibi yao kwenye mji wa Kakamas, Kaskazini mwa Mkoa wa Cape siku ya Jumanne.

Katika tukio jingine watoto wawili walikufa kwa kukosa hewa baada ya kufungiwa kwenye gari ambalo lilikuwa linangojewa kufanyiwa matengenezo Jijini Johannesburg.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni