Mbunge wa jimbo la Bumula nchini
Kenya Bw. Boniface Otsiula ametoa kali ya mwaka baada ya kuwataka
wanawake katika jimbo lake kujifungua watoto wengi wawezavyo ili
kulijaza jimbo hilo.
Mbunge Otsiula amesema jimbo hilo
linaidadi ndogo ya watu, kutokana na ukweli kuwa wanawake wengi
wanatumia njia za mpango wa uzazi zinazowafanya washindwe kuzaa na
kuongeza idadi ya wapigakura ambayo ni ndogo kwa sasa.
Akiongea kwenye shule ya Sekondari
ya Ng'oli mwishoni mwa wiki, Bw. Otsiula mesema jimbo hilo linahitaji
kuwa na watoto wengi, ambao watakapokuwa watakuwa wapigakura badala
ya kuwauwa kwa mbinu za mpango wa uzazi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni