.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 24 Januari 2016

MCHEKESHAJI CHRIS ROCK HATOSUSIA KUSHEREHESHA TUZO ZA OSCARS

Mchekeshaji nyota Chris Rock atasherehesha hafla ya utoaji tuzo za Oscars, licha ya kuwepo kwa uvumi kwamba atajiondoa kutokana na waandaaji wake kudaiwa kuonyesha upendeleo kwa waigizaji filamu weupe.

Prodyuza wa Tuzo za Oscars, Reginald Hudlin, akiongea wakati wa uteuzi wa tuzo za 47 za NAACP jumamosi Jijini Los Angeles amesema kuwa Rock, 50, atatekeleza majukumu yake ya ushereheshaji tuzo hizo Februari 28.

Mchekeshaji huyo ambaye pia ni muigizaji filamu atasherehesha tuzo hizo za Oscars, huku baadhi ya wasanii wa tasnia ya filamu wenye asili ya Afrika kama, Muongoza filamu Spike Lee, waigizaji Jada Pinkett Smith, na Will Smith wakihamasisha kususiwa tuzo hizo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni