Waziri Mkuu wa Sweden ameelezea
tukio la kuchomwa kisu na kufa mfanyakazi mwanamke kwenye kituo cha
kuhifadhia wahamiaji kuwa ni uhalifu wa kutisha.
Waziri Mkuu huyo Stefan Lofven
ametembelea kituo hicho cha wahamiaji watoto wasio na waangalizi
kilichopo Molndal, karibu na Gothenburg, saa kadhaa baada ya mauaji
hayo.
Mtuhumiwa ambaye ni mhamiaji
anayetafuta hifadhi mwenye umri wa miaka 15, amekamatwa kwa kumuua
mwajiriwa mwenye umri wa miaka 22.
Maafisa wa usalama wa Sweden wakiwa katika nyumba iliyotokea tukio hilo la mauaji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni