Mwanzilishi mkongwe wa mazoezi ya
yoga ya joto nchini Marekania ameagizwa kulipa zaidi ya dola milioni
6 kwa wakili mwanamke ambaye alimdhalilisha kingono na kumfukuza kazi
kuchunguza tuhuma hizo.
Mwanzilishi huyo milionea Mmarekani
Bw. Bikram Choudhury, 69, ni maarufu kwa mbinu za yoga na alianza
kufanya mazoezi ya yoga tangu mwaka 2002.
Fidia hiyo ya dola milioni 6 ni
nyongeza ya dola milioni moja iliyotolewa kwa mwanamke huyo Minakshi
Jafa-Bodden ambaye alikuwa ni mwanasheria na afisa uhusiano wa
kimataifa wa Bw. Choudhury Jijini Los Angeles mwaka 2011 hadi 2013.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni