Polisi Kenya inamshikilia mwanamke
anayedaiwa kumuua mwanaume wake kwa kumchoma kisu, kufuatia ugomvi
uliosababishwa na mvutano wa kuangalia programu za televisheni.
Kamishna wa Polisi wa Nairobi Kaunti
Japhet Koome, amesema mwanamke huyo wa miaka 27 aitwae Caroline
alimchoma mpenzi wake mwenye umri wa miaka 25 siku ya jumanne usiku.
Bw. Koome amesema wapenzi hao wawili
walikuwa wanagombea remoti kila mtu akitaka kuangali programu tofauti
na ndipo mwanamke alipochukua kisu jikoni na kumchoma nacho mwanaume
tumboni na kwenye paja.
Ugomvi huo ulitokea saa nne usiku
wakati chaneli moja televisheni ilipokuwa ikionyesha tamthilia na
nyingine ikionyesha mechi ya mpira miguu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni