Nchi ya Liberia itatangazwa kutokuwa
tena na maambukizi ya Ebola na Shirika la Afya Duniani (WHO), na
kumalizika kwa mlipuko mbaya zaidi kuwahi kutokea wa ugonjwa huo
duniani.
Hatua ya kumalizika kwa matukio ya
ugonjwa wa Ebola Liberia itatangazwa baada ya siku 42 bila ya kuwepo
kwa tukio la mgonjwa wa Ebola.
Liberia itaungana na mataifa ya
Guinea na Sierra Leone, ambazo zilitangazwa kutokuwa tena na
maambukizi ya Ebola mwaka jana. Ebola iliuwa watu 11,000 tangu
Desemba 2013.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni