.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 20 Januari 2016

MWANAMKE KENYA ACHOMWA MOTO KWA KUSOMA UJUMBE WA SIMU YA MUMEWE

Mwanamke Dorcas Awinja wa nchini Kenya anauguliwa majeraha ya kuchomwa moto na mumewe kwa kutumia mafuta ya taa, kutokana na ugomvi wa kusoma ujumbe wa simu wa nyumba ndogo kwenye simu ya mumewe.

Awinja, amelazwa kwenye hospitali ya Nairobi tawi la Nakuru mwili wake ukiwa umeungua kwa asilimia 63, huku akiwa na majeraha ya kuungua na moto kwenye shingo, mkono, titi, tumbo na miguuni.

Akisimulia kisa hicho Awinja amesema wakati wakianza kulala simu ya mumewewe iliita bila ya kupokelewa na ndipo alipoichukua ukaingia ujumbe wa mapenzi, uliomfanya apandwe hasira na kuibua ugomvi, ulioishia yeye kuchomwa moto na mumewe.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni