Nyumba ya nguli wa filamu George
Clooney na mkewe mwanasheria wa haki za binadamu, Amal waliyoinunua
kwa kiasi cha paundi milioni 10, inanyemelewa na mafuriko baada ya
mto Themes kujaa maji na kupasuka kingo zake.
Nyumba hiyo ya nyota huyo wa filamu
na mkewe iliyopo katika kijiji karibu na Reading, Berkshire nchini
Uingereza ilikuwa imeshafanyiwa ukarabati wa vyumba vyake tisa, na
sasa ipo hatarini iwapo mto Themes utafurika zaidi.
Kina chama maji cha mto Themes
kimeongezeka mno baada ya wiki kadhaa za mvua na Mamlaka ya Mazingira
Uingereza imeonya kutokea mafuriko katika maeneo yaliyo mabondeni hii
leo.
Maji ya mafuriko yakiwa yameshafika kwenye eneo la bustani la nyumba ya George Cloone
George Clooney akiwa na na mkewe Amal



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni