Rais wa Senegal, Macky Sall
amependekeza kupunguza muda miaka miwili katika muhula wake wa urais
katika hatua za kuimarisha Demokrasia.
Kubadili muda wa muhula wa urais
kutoka miaka saba hadi mitano ni sehemu ya mapendekezo ya mabadiliko
ya Katiba ambayo yatapigiwa kura ya maoni.
Wakati rais Sall akipinguza muda
wake wa urais, marais wa mataifa mengine kadhaa ya Afrika hivi
karibuni wamekuwa wakibadili Katiba ili kuongeza muda wa kuendelea
kukaa madarakani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni