.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 27 Januari 2016

SI KWELI KWAMBA RAIS MAGUFULI KUZURU KENYA KUHUDHURIA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU JARAMOGI ODINGA NA FIDEL ODINGA

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii.

Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanahabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe.

Haijulikani ni nini hasa nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!

Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni