.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Januari 2016

UTAFITI WABAINI WANAUME WENGI WA MIKOA YA NAIROBI NA NYANZA HUPIGWA NA WAKE ZAO

Utafiti uliofanywa nchini Kenya umeonyesha kuwa wanaume wa mikoa ya Magharibi, Nairobi na Nyanza wanaongoza kwa kukabiliwa na vitendo vya kunyanyaswa, kudhalilishwa na kupigwa na wake zao.

Utafiti huo ambao ulikuwa ukijaribu kupigana na mtazamo kuwa wanaume wa mkoa wa Kati Kenya wanakabiliwa zaidi na vitendo vya ukatili na vipigo kutoka kwa wanawake wao, umebaini nusu ya wanaume waliohojiwa katika mikoa hiyo wamepata vipigo, kudhalilishwa kingono na kuthiriwa hisia zao na wake zao.

Matokeo ya utafiti huo yametolewa jana katika uzinduzi wa utafiti wa idadi ya watu na hali ya afya, uliofanywa mwaka 2014, unaolenga kuangalia idadi ya watu Kenya pamoja na hali za afya za wananchi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni