Mshambuliaji wa Manchester United,
Wayne Rooney amefanikiwa kuizima Liverpool nyumbani baada ya kufunga
bao pekee katika dakika ya 78 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Ikicheza kwenye dimba la nyumbani la
Anfield Liverpool ilifanya mashambulizi makali katika nusu ya kwanza
ilioishia kila timu kutoona nyavu za mwenzake.
Mchezaji Adam Lallana alikosa nafasi
nzuri ya Liverpool katika nusu ya kwanza, ambapo Emre Can akinyimwa
bao katika kipindi cha pili.
Wayne Rooney akimtoka beki wa Liverpool Kolo Toure
Kipa wa Man Utd David De Gea akimnyima goli Lallana
Ashley Young aliumia katika mchezo huo mnano dakika ya 43




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni