Askari wanne wa Jeshi la Ulinzi
Kenya waliojeruhiwa wakati wa mashambulizi yaliyofanywa na Al-Shabaab
katika kambi yao iliyopo Somalia wamesafirishwa kwa ndege hadi
Nairobi kwa kutumia ndege binafsi.
Wanajeshi hao ambao wote ni wanaume
wamepokewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Kenya Jenerali Samson
Mwathethe, Kamanda wa Jeshi Luteni Jenerali Leonard Ngondi, Kamanda
wa Kikosi cha Anga Kenya Samuel Thuita na Waziri wa Ulinzi Raychelle
Omamo.
Wanajeshi hao wanne wameokolewa
nchini Somalia baada ya kutembea kilomita kadhaa kutoka kwenye kambi
ya El-Adde iliyopo Gado ambapo kundi la Al-Shabaab lilifanya
shambulizi siku Ijumaa.
Askari watatu waliweza kutembea
wenyewe bila ya msaada wowote kutoka kwenye ndege kwenda kwenye gari
la wagonjwa na mmoja wao alibebwa kwenye machela ambaye inasemekana
ameumia vibaya kiunoni.
Mwanajeshi wa Kenya akiwa amelazwa kwenye machela baada ya kuletwa Nairobi


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni