Papa Francis amewasalimia maelfu ya
wahamiaji katika uwanja wa St Peter huko Vatican, wakati Kanisa
Katoliki likiadhimisha siku ya wakimbizi.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki
Duniani, amewaambia wahamiaji hao kuwa wamebeba historia, utamaduni
na maadili bor, huku akiwataka wasikate tamaa.
Wahamiaji hao wengi wao wakiwemo
wanaoomba hifadhi walikuwa wakipeperusha bendera za mataifa yao
wakati Papa Francis alipokuwa akiwahutubia.
Mataifa ya Ulaya yamekuwa yakihaha
katika kumudu kukabiliana na wimbi la kasi ya ongezeko la wahamiaji.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni