Bondia Carl Frampton amemdunda Scott
Quigg kwa uamuzi wa kura uliotofautiana na kufanikiwa kuunganisha
mikanda miwili ya IBF na WBA uzito wa super-bantamweight katika
ubingwa wa dunia.
Katika mchezo huo ambao majaji
walionekana kutofautiana, majaji wawili walimpa Carl Frampton pointi
116-112 huku jaji mmoja akimpatiwa Scott Quigg pointi 115-113.
Kwa ushindi huo rekodi ya sasa ni
mapambano 22 akishinda yote ambapo 14 kati ya hato ni kwa KO, wakati
Quigg akipambana mara 34 kushinda 31 ambapo 23 kati yake ni kwa KO,
kutoa sare mara mbili na kupoteza mara moja.
Bondia Carl Frampton akimpiga ngumi ya kifuani Scott Quigg



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni