TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABAR
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha
sh. bilioni 1.65/- kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya
walimu hapa nchini.
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati
akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya
zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu
Mtwara.
"Serikali inatambua uhumimu wa mafunzo kwa vitendo katika
vyuo vya ualimu ni kwa sababu hiyo mwezi huu wa Februari tumetoa sh.
bilioni 1.65/- kwa vyuo vya ualimu 35 vya umma nchini ili kuwezesha
wakufunzi na walimu wanafunzi kushiriki kikamilifu mafunzo kwa
vitendo (Block Teaching Practice)," alisema huku akishangiliwa.
Alisema fedha hizo zinapaswa zitumike kulipia posho za
kujikimu, nauli na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Mapema, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa, Waziri Mkuu alisema
Serikali imedhamiria kuimarisha elimu na akawaonya wote
wanaowaharibia elimu watoto wa kike.
"Tunataka watoto wa kike wasome wa Kitanzania wasome hadi
elimu ya juu waje wawe watumishi wa umma hapo baadaye. Kila mmoja awe
mlinzi wa mwenzake tukikumbuka kaulimbiu ya Mama Salma Kikwete ya
kwamba 'Mtoto wa Mwenzio ni wako'," alisema.
"Yeyote atakayemharibia mtoto wa kike masomo kwa
kumrubuni na chips au pipi ajiandae kwenda Lilungu, (gereza la mkoa
wa Mtwara)", alisema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni