.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 8 Februari 2016

GHARIKA IMOGEN YASABABISHA MAAFA UINGEREZA

Nyumba zaidi ya 13,000 zimeachwa bila umeme leo kufuatia gharika Imogen kuikumba Uingereza ikiambatana na upepo wenye kasi ya 100mph.

Gharika hiyo imeathiri eneo la kusini na kuwafanya wasafiri wawe na wakati mgumu, wakati watoto wawili wakikimbizwa hospitali baada ya ukuta kuwaangukia.

Kumetolewa tahadhari za mafuriko zaidi ya 280 huku huko Wales malori yakizingira na maji huku mvua kubwa zaidi ikitarajiwa kunyesha leo.
                      Meli ikiwa inapigwa na wimbi kubwa lililoambatana na gharika
                        Gari lililosombwa na upepo wa gharika likiwa limeanguka chini
         Maafa miti nayo haikusalimika kama inavyoonika hapa ukiwa umeangukia gari

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni