Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon amewasili Juba katika kujaribu kufufua makubaliano ya amani
ambayo yamekwama ili kumaliza miaka miwili ya mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe nchini Sudani Kusini.
Ki-moon alipokelewa jana uwanja wa
ndege wa Juba na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Barnaba Marial
Benjamin na kisha kupelekwa kuonana na rais Salva Kiir ambaye tafauti
zao na mpinzani wake Riek Machar ziliibua machafuko tangu Desemba
2013.
Mapigano yanaendelea licha ya
makubaliano ya amani ya Agosti mwaka jana ambapo watu wapatao 18
wameuwawa katika tukio la hivi karibuni kaskazini mashariki mwa mji
wa Malakal wiki iliyopita.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni