Kundi la wahamiaji limevunja kizuizi
cha fensi ya waya zenye kuchoma kwenye mpaka wa Macedonia na Ugiriki
wakitumia vyuma kuvunja uzio huo.
Picha za TV zimeonyesha wahamiaji
wakisukuma uzio huo huko Idomen, na kuzikata nywaya za kuchoma huku
polisi wa Macedonia wakitumia mabomu ya machozi kuwatimua.
Haijafahamika mara moja wahamiaji
wangapi wameweza kuvuka, ambapo wengi wao wanataka kufika nchi za
Ulaya wakitokea Syria na Irak.
Wahamiaji wakisukumana na polisi wenye ngao za kioo baada ya kuvunja uzio huo
Mtoto akiangua kilio wakati wa ghasia hizo zilizoambatana na mabomu ya machozi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni