Waziri wazamani wa mambo ya ndani wa Nigeria amefunguliwa
mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kuhusiana na
zoezi la ajira lililopelekea watu kukanyagana na kusababisha vifo vya
watu 20.
Waziri huyo Abba Moro aliongoza zoezi hilo la kuwahamasisha wahitimu vijana
wa vyuo vikuu kuomba nafasi za ajira kwenye idara ya uhamiaji mwaka
2014.
Uwanja uliotumika kwa usahili wa vijana wanaoomba ajira
ulizidiwa na watu waliojitokeza kuomba ajira.
Bw. Moro amekiri kosa la kuhusika na kujipatia fedha kiasi cha
dola milioni 2.5 kwa njia za udanganyifu zinazohusina na ada ya
maombi ya kazi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni