.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 7 Februari 2016

MAELFU YA MASHABIKI WA TIMU YA LIVERPOOL WATOKA NJE KUGOMEA BEI MPYA YA TIKETI

Maelfu ya mashabiki wa timu ya Liverpool walitoka nje ya uwanja wao jana wakati wa mchezo wao na Sunderland katika dimba la Anfield kupinga kuongezwa kwa gharama za tiketi.

Kundi hilo la mashabiki wa Liverpool liliwahamasisha mashabiki kuondoka uwanjani dakika ya 77 ya mchezo huo kupinga bei ya tiketi ya gharama ya juu kuuzwa paundi 77 kwenye dimba lao jipya katika msimu ujao.

Katika mchezo huo ulioishia kwa sare ya mabao 2-2 mashabiki wa Liverpool walitoka uwanjani wakiimba wimbo wa klabu hiyo wa 'You'll Never Walk Alone', huku wakipaza sauti kwa kusema bei hiyo mpya haiwezekani.
   Shabiki wa Liverpool anayepinga bei mpya akiwa na ujumbe unaosema ni aibu paundi 77

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni