Mpango ya rais Barack Obama ya
kudhibiti uchafuzi wa hewa ya ukaa kutoka kwenye mitambo ya nishati
ya umeme ya Marekani umekwamishwa kwa muda na Mahakama ya Juu ya nchi
hiyo.
Mahakama imesema mpango wa rais
Obama wa matumizi ya nishati isiyochafua hewa, hauwezi kutekelezwa
hadi hapo pingamizi la kisheria lililowasilishwa litakaposikilizwa.
Mpango huo wa rais Obama umeandaliwa
kupunguza uchafuzi wa hewa Marekani kwa sailimia 32 ifikapo 2030,
huku ukisisitiza matumizi ya nishati jadifu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni