Vyombo vya habari nchini Korea ya
Kusini vimetangaza kwamba mnadhimu wa jeshi la Korea Kaskazini Ri
Yong-Gil amenyongwa ikiwa ni mfululizo wa matukio ya kuuwawa kwa
viongozi waandamizi wa nchi hiyo chini ya utawala wa kiongozi wa nchi
hiyo Kim Jong-Un.
Taarifa ya vyombo hivyo vya habari
zinasema mnadhimu huyo alinyongwa mapema mwezi huu kwa madai kuwa
aliunda kikundi cha upinzani na kujihusisha na rushwa.
Taarifa hiyo imetoaka wakati kukiwa
na mtafaruku kati ya Korea Kusini na Kasikazini juu ya mvutano wa
kisiwa cha Peninsula na Korea Kasikazini kurusha makombora ya masafa
marefu na kufanya majaribio ya nyuklia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni