Umoja wa Kujihami wa Nato upo tayari
kufanya doria kwenye bahari ya Aegean kuwadhibiti watu wanaowavusha
kimagendo wahamiaji kutokea nchi ya Uturuki kuingia Ugiriki
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashton
Carter ametoa tangazo hilo kufuatia ombi kutoka nchi wanachama wa
Nato za Uturuki, ujerumani na Ugiriki.
Wakati Mawaziri wa ulinzi wa Nato
wakikutana Jijini Brussels, mipango inaandaliwa ya kuwa na jeshi la
ushirikiano ili kutekeleza mpango huo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni