.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 11 Februari 2016

WAVAMIZI WENYE SILAHA KATIKA ENEO LA OREGON MAREKANI KUONDOKA

Wavamizi wanne wenye silaha katika eneo la hifadhi ya wanyamapori ya Marekani katika jimbo la Oregon wanajiandaa kujisalimisha, mmoja wa wanachama wa kundi hilo amesema.

Mwanachama huyo Sean Anderson amesema wavamizi hao wenye silaha wataondoka kwenye jengo la Malheur leo, katika tangazo alilolirusha kwa njia ya intaneti.

Mapema makachero wa Shirika la Ujasusi la Marekani FBI, walilifikia kundi hilo ambalo lilikuwa limejificha kwenye mitaro kwa siku 40.

Watu hao wanapinga serikali ya shirikisho kwa kuchukua eneo hilo la hifadhi ambalo wanadai kuwa ni lao tangu asili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni