Muwania urais wa Marekani kwa tiketi
ya chama cha Republican Bw. Donald trump ameshinda kura za maoni
South Carolina, na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuteuliwa na
chama chake kuwania urais.
Katika kinyang'anyiro hicho kwa
upande wa wagombea wa chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton
amemshinda Bernie Sanders kwenye mchakato wa kura ya maoni uliokuwa
na ushindani mkali.
Matokeo hayo yote mawili yatakuwa ni
muhimu kuelekea siku ya jumanne ya Machi mosi ambapo makumi ya
machimbo yataamua nani anafaa kuwania urais wa Marekani.
Ushindi wa Bw. Trump umepelekea
kummaliza kabisa Gavana Jeb Bush ambaye ameondoka kwenye mbio za
kuwania urais kwa chama cha Republican.
Donald Trump akiweka mkono juu ya ujauzito wa binti yake Ivanka


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni