.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 11 Februari 2016

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH.ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKAA WA 25 WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF

Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachamana wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko" unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.

Baadhi ya Wadau washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju alipokuwa akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko",unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wanachama wa Mfuko wa PPF mwenye ulemavu wa kusikia akiendelea kufatilia mada mbali mbali kwenye mkutano huo kupitia mkalimani wa lugha ya alama.
Wadau wakipitia kablasha la PPF













Hakuna maoni :

Chapisha Maoni