Mwanamuziki Sir Elton John, ameweza
kupata ujasiri wa kumuomba msamaha mama yake mzazi Sheila
Farebrother, 90, baada ya kutangaza hadharani kuwa wamemaliza ugomvi
wao uliodumu kwa miaka minane.
Mwanamuziki huyo alifanikisha
kumaliza tofauti zake na mama yake pale alipomtumia shada la mauwa
meupe la bei mbaya, mwaka jana, wakati mama yake Sheila alipokuwa
ametimiza umri wa miaka 90.
Zawadi hiyo ya shada iliambapata na
maandishi yaliyoandikwa 'Wow, 90! Congratulations. Love Elton, David,
Zachary and Elijah,' ikiwa ni mawasiliano yao ya kwanza kufanyika
baina yao baada ya ukimya wa miaka saba.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni