| Wakulima wakiwa katika mafunzo hayo. |
| Wakulima wakiwa katika mafunzo ya kupiga picha. |
Na Dotto Mwaibale
JUKWAA la Bioteknolojia (OFAB) limetoa mafunzo ya kutumia simu katika kupashana habari kwa wakulima wilayani Butiama mkoani Mara ili kuwarahisishia kazi zao za kilimo.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika Kijiji cha Kisamwene wilayani humo ili kuwasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.
"OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida" alisema Nyinondi.
Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.
Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 28 kutoka Kata tano zilizopo wilayani Butiama mkoani humo na yaliwahusisha viongozi wa vijiji, kata na wenyeviti wa serikali za mitaa.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni