Mhe. Kitwanga alisema wanaotumia mtandao wanawajibu wa kutumia mtandao kwa matumizi ambayo hayatavunja sheria na ambao watakuwa wakikiuka sheria hiyo serikali haitawavumilia na watawachukulia hatua za kisheria.
Adhabu ya kuvunja sheria hii ya makosa ya mtandao ni mbaya sana na
ninataka kuwambia Watanzania wazingatie sheria za mtandao … kifungo ni
miaka 30 au hata zaidi,” alisema
Kitwanga.
Aidha aliwataka ambao wamekuwa wakitukanwa
katika mitandao ya kijamii wapeleke malalamiko Polisi na serikali
imejipanga kuwachukulia hatua watumiaji ambao wamekuwa hawafati sheria
za mtandao.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa
msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba alisema kuwa jeshi hilo limekuwa
likiwachukulia hatua watumiaji wote wa mitandao ambao wamekuwa wakikutwa
na hatia ya kufanya matumizi
mabaya.
Alisema tangu imetungwa sheria hiyo
wameshafungwa baadhi ya watumiaji na kesi saba zikiwa mahakamani na bado
wanaendelea kufatilia watumiaji wengine ili wawachukulie
hatua.
“Polisi tunaendelea kuwachukulia hatua
watumiaji ambao wanakuwa na makosa na kwasasa kuna kesi saba zipo
mahakamani … tangu sheria imetungwa kesi tunazopokea zinazohusu mitandao
zimepungua kutoka 25 hadi 30 kwa siku ila siku hizi zinakuwa 10 au
chini ya hapo,” alisema Bulinda.
Nae mmoja wa watumiaji wa mtandao, Grace
Mwanga aliwashauri Watanzania wenzake kudumisha maadili ya kitanzania na
kuifanya mitandao kama njia ya mawasiliano kama jinsi lilivyo kusudiwa
na waanzilishi wa mitandao hiyo.
“Watanzania tudumishe maadili yetu ya zamani,
mitandao isitufanye tusahau asili yetu … tutumie mitandao kuwasiliana
na hata kufanya matangazo ya biashara zetu,” alisema Grace.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni