Chelsea imefanikiwa kutinga robo
fainali ya FA baada ya Diego Costa, Willian, Gary Cahill na Eden
Hazard kufumania nyavu katika mchezo walioibuka na ushindi mnono wa
mabao 5-1 dhidi ya makinda wa Manchester City.
Katika mchezo huyo mshambuliaji
hatari Diego Costa alifunga goli la kwanza kabla ya David Faupala
kuisawazishia Manchester City. Willian na Gary Cahill walifunga
magoli na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa mabao 3-1.
Eden Hazard aliongeza bao la nne kwa
mkwaju wa mpira wa adhabu karibu na eneo la penati, Oscar akapoteza
penati katika dakika ya 75, kabla ya Bertrand Traore kukamilisha
karamu ya magoli katika dakika ya 89.
Diego Costa akifunga bao kwa kichwa cha kupiga mbizi
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich akionekana kuridhika na matokeo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni