.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Machi 2016

AMUUA BABA YAKE KWA KULA UGALI WAKE ALIOBAKISHIWA NA MAMA

Mwanamke mmoja jana ameiambia mahakama nchini Kenya kuwa mtoto wake wa kiume ndiye aliyemuua baba yake kutokana na kula sahani ya ugali aliowekewa.

Mwanamke huyo Christine Lumbukhu ametoa ushahidi huo katika Mahakama Kuu ya Kakamega, kuwa mtoto wake wa kumzaa Vincent Makhalasia, alimuua baba yake Atanas Matayos, Julai 12, mwaka 2013 kijijini kwao Mundulu.

Mtoto huyo wa kiume alikesha kwenye msiba, na mama yake alimuachia ugali wake wa mlo wa usiku lakini hakurudi hadi asubuhi na alipofika nyumbani aliulizia mlo wake ndipo alipoambiwa baba yake kala ndipo alipomshambulia na kumsababishia kifo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni