.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 9 Machi 2016

BOBAN,KENNY ALLY KUIKOSA STAND UNITED

Kiungo Haruma Moshi Boban atalazimika kusubiri mpaka Marchi 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City kufuatia kusumbuliwa na maralia jambo linalomfanya kuukosa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Stand United ya Shainyanga uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Muda mfupi uliopita mkuu wa kitengo cha utabibu kwenye kikosi cha City, Dr Joshua Kaseko ameifahamisha mbeyacityfc.com kuwa mara baada ya kikosi kizima kurejea Mbeya kutoka jijini Dar kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba, alipata taaraifa ya kutokuwa katika hali nzuri kwa kiungo huyo na baada ya kumfanyia vipimo aligundua kuwa Boban ana Maralia.

“Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo kesho,ana Maralia tumeshamtaarifu mwalimu juu ya hili na tayari ameanza kufanya mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans Sports jijini Tanga alisema.

Katika hatua nyingine Dr Kaseko alidokeza kuwa kiuongo mwingine wa kati, Kenny Ally Mwambungu ataukosa mchezo wa kesho kupisha kadi tatu za jano alizopata mfululizo kwenye michezo mitatu ya City iliyopita, na kukumbumbusha pia kuwa mlinzi Deo Julius bado atakuwa nje ya kikosi akiendelea kuuguza majeraha ya goti.

“Kwenye mchezo wa kwesho pia tutawakosa Kenny Ally na Deo Julius kutokana na sababu kadha wa kadha, Kenny amepata kadi tatu za njano mfululizo kwenye michezo yetu mitatu iliyopita na Deo bado hajapona majeraha ya goti hivyo nao hawatakuwa sehemu ya mchezo hapo kesho”alimaliza

City inakutana na Stand United hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine huu ukiwa ni mchezo wa nne kwa timu hizi huku rekodi ikionyesha timu hiyo ya Shinyanga kushinda mara mbili na City ikiwa imeshinda mara moja, hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni