Timu ya Arsenal imemaliza nuksi ya kucheza michezo mitano bila
ya kushinda baada ya kuchapa Hull City kwa mabao 4-0 katika mchezo wa
raundi ya tano wa kombe la FA, na kutinga robo fainali ambapo
itakutana na Watford.
Arsenal walipatiwa zawadi ya goli la kwanza na beki wa Hull
City, David Meyler aliyemuandalia kimakosa mpira Olivier Giroud
ambaye naye bila ajizi akapachika bao la kwanza, na baadae Aaaron
Ramsey naye nusura ajifunge na kuisaidia Hull kusawazisha.
Giroud alipachika bao la pili kwa Arsenal huku naye Theo
Wallcott akipachika la tatu na kukamilisha karamu kwa kufunga bao la
nne.
Olivier Giroud akifunga bao kwa kupitisha tobo kwenye miguu ya kipa
Theo Wallcott akipiga mpira wa kuzungusha na kuandika bao la nne
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni