Bondia Nick Blackwell alikimbizwa hospitali baada
ya kupigwa na Chris Eubank Jr katika pambano la uzito wa uzani wa
kati nchini Uingereza lililofanyika jana Jijini London.
Refa wa pambano hilo alilazimika kulisimamisha
katika raundi ya 10, baada ya daktari kushauri Blackwell hatoweza
kuendelea kutokana na uvimbe kwenye jicho lake la kushoto.
Bingwa huyo aliyedundwa baadaye alilazimika
kuondolewa kwenye ulingo kwa kutumia machela na kukimbizwa hospitali
kwa matibabu.
Refa akiwa amemshika Nick Blackwell aliyekuwa akivuja damu kwa kipigo
Bondia Nick Blackwell akipingwa ngumi ya kushoto na Chris Eubank Jr
Chris Eubank akifurahia ushindi wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni