Wachezaji wa zamani wa Manchester
United Cristiano Ronaldo na Luis Nani wamepachika bao kila mmoja na
kuing'arisha Ureno katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Ubelgiji ulioishia kwa ushindi wa mabao 2-1.
Katika mchezo huyo mshambuliaji wa
timu ya Everton na Ubelgiji, Romelu Lukaku, alifunga bao pekee kwa
timu yake, lililotokana na krosi iliyopigwa na ndugu yake Jordan, na
kulifanya goli hilo kuwa ni la hisia za aina yake wakati wakifurahia.
Luis Nani akiwa ameruka sarakasi angani kushangilia goli alilofunga
Romelu Lukaku na ndugu yake Jordan wakikumbatiana kushangilia goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni