Timu ya Uingereza iliyojaa matumaini
baada ya ushindi dhidi ya Ujerumani imejikuta ikifungwa mabao 2-1
katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uholanzi ambayo
haikufuzu michuano ya Euro 2016.
Katika mechi hiyo ya jana usiku
iliyopigwa kwenye dimba la Wembley timu hizo zilisimama kucheza
katika dakika ya 14 ili kutoa heshima kwa mchezaji wa zamani nyota
Johan Cruffy aliyefariki dunia.
Janssen akifunga goli la penati na kumpoteza kipa Fraser Forster
Jamie Vardy akifurahi bao alilofunga akiwa na Kyle Walker
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni